Do you like Humaniq Farm?
Subscribe to learn about new articles first
Write Close
Close
Contact us!
Msaada na motisha kwa mkulima wa Tanzania
Mkono wa msaada kwa wakulima

English | Swahili
Makala na: Jensen Tom | 6 august 2018
Kazi ya ukulima Tanzania ni mojawapo ya kazi muhimu kwani takwimu za serikali zinaonesha shughuli za kilimo zinatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 50 ya wananchi. Kuna kilimo cha mazao ya chakula, kilimo cha mazao ya biashara na kilimo cha matunda na mbogamboga. Tanzania ina maeneo ya miji machache hivyo kwa wingi kilimo kinafanyika vijijini ambapo ndio kuna maeneo makubwa na idadi kubwa ya wakazi. Unaweza kusema wakulima wengi wa Tanzania bado hawajaweza kutumia kilimo cha kisasa kwenye uzalishaji wao. Kuna jitihada nyingi za kumkomboa mkulima wa Tanzania na kumleta katika karne mpya ya mabadiliko ya kiteknolojia. Nafasi za wanaotaka kuanza kujihusisha na kilimo zipo na pia kuna misaada katika mfumo wa mikopo wa fedha, vifaa na elimu.

Je unataka kufahamu kuhusu aina za mazao yanayolimwa Tanzania? 'SHARE' ukurasa huu kisha nenda sehemu ya maoni apo chini na utuandikie au utuulize swali
Serikali
Ikiwa kama sekta ambayo imetoa ajira kwa karibu asilimia 65 ya wananchi wa Tanzania na kuchangia takribani nusu asilimia ya pato la taifa, serikali ndio mstari wa mbele kwenye kutoa msaada kwa wakulima wa Tanzania. Karibu maeneo yote serikali imejikita na nia haswa ikiwa ni kukuza kilimo na kumsaidia mkulima kuendana na mabadiliko.

Kuna mradi kama ASDP II (Agricultural sector development program) chini ya sera ya KILIMO KWANZA unaomsaidia mkulima kuondokana na upoteaji wa mazao ya nafaka kipindi cha mavuno na kuboresha miundombinu ya barabara na uhifadhi kama maghala. Hatua kama kuondoa ushuru kwenye usafirishaji wa mazao yanayozalishwa nchini inalenga kumpunguzia gharama mkulima anaezalisha bidhaa nchini na anataka kufikisha bidhaa yake sokoni kwa urahisi.

President of Tanzania Dr.Magufuli launching ASDP II (Photo by Daily News)
Serikali bado imekua ikihimiza wakulima kuanzisiha au kujiunga na vikundi vya ushirika kama SACCOS (savings and credit cooperatives) na vikundi vya VIKOBA ili kurahisisha kupata msaada ya mikopo isiyo na masharti mengi. Mfano benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Development Bank - TADB) inafanya kazi na vikundi vya ushirika SACCOS ambavyo vinapatikana karibia kila kona ya Tanzania kutoa mikopo ya muda mfupi na muda mrefu kwa wakulima wenye uhitaji. SACCOS ni vikundi vya ushirika vya akiba na mikopo vinavosimawa na na kusajiliwa kisheria katika wilaya zote. Vinaanzishwa kwa kundi lolote la watu kuanzia 5 wenye nia inayofanana mfano wakulima, wavuvi, walimu kwa ajili ya kukopeshana au kufanya ujasiriamali na kisha kugawana faida ili kujiinua kiuchumi. Takwimu zinaonesha serikali imeendelea kuongeza fedha kwenye vikundi hivi kutoka shilingi bilioni 855 mwaka 2016 hadi shilingi bilioni 902 mwaka jana.

Serikali inaendesha tafiti nyingi zinazomlenga mkulima kwa kupata mbegu bora, kuondoa na kupiga marufuka madawa na mboloea ambazo zina kemikali hatarishi kwa ardhi afya ya mkulima na afya ya matumiaji wa mwisho. Elimu ya tafiti hizi na njia bora za kilimo zinatolewa kwenye maonesho kama nanenane na sababa, mitandao na vituo mbali vya serikali na wadau binafsi wa sekta ya kilimo. Mkulima yoyote anaweza kupata msaada kwenye maonesho hayo au kwenda ofisi za wilaya na kuonana na kitengo cha kilimo. Tafiti hizi zinaendana na ubunifu kwa utumiaji wa teknolojia kwenye kupata matokeo chanya kwenye kilimo

Je una swali, maoni au ushauri kwenye jitihada za serikali kwa mkulima? Bofya 'SHARE' na kisha tuandikie kwenye sehemu ya maoni apo chini.
Mchango wa sekta binafsi na msaada wa Kigeni

GAFCO envisions Tanzanian farmers feeding the world (Photo from VisionFund)
Kuna miradi mingi ya mashirika binafsi na ya kimataifa inayolenga kumpatia mkulima wa Tanzania misaada kama elimu, misaada ya kifedha na teknolojia na mingine mingi kwa kufanya kazi na wakulima, wakala au kupitia ofisi za serikali za vijiji ambapo miradi mingi inafanyika. Ili kufikia mkulima ambae haumjui inakua rahisi kutumia ofisi za kijiji kwani ofisi hizi ndio zinatambua nani anajishughulisha na kilimo na vipi wanaweza kuwafikia. mkulima unaweza kujipatia msaada wa mashirika ambao hutolewa bila malipo kama yapo kwenye kijiji chako, cha muhimu ni kuhudhuria warsha zao na kusikiliza namna unavoweza kujipatia misaada ya elimu, mikopo au vifaa . Ukurasa wa shirika lisilo la kifedha WORLD VISION linaonyesha mpaka sasa wanafanya kazi mikoa zaidi ya 10 Tanzania na wameanzisha shirika la biashara, GAFCO (Great African Food Company) na miongoni mwa misaada kwa mkulima mdogo ni kusaidia kuuza mazao kama mtama na mahindi kwenye soko la ndani na mazao kama maharage na mbegu za maua nje ya Tanzania.
Mashiriki haya yamejaribu kumsogezea mkulima huduma kwa ukaribu bila masharti mengi ukifananisha na misaada au mikopo ya biashara zingine ambazo sio za kilimo. Shirika lingine kama EFTA (Equity for Tanzania) linatumia mawakala au wasambazaji wa vifaa vya kilimo kutoa mikopo ya mashine kama matrekta bila dhamana kwa wakulima. Mkulima yoyote anaweza kufika kwenye ofisi zao au kuwasiliana na mawakala wao amabao wanaonekana kwenye mtandao wao ili kujipatia huduma zao.
Msaada wa Jamii kwa mkulima
Mchango wa jamii kwa mkulima umekua kwa asilimia kubwa ni kujihusisha na jitihada za kilimo kwa mfano kwa kukodi shamba binafsi kwa wakulima ambao hawana umiliki wa ardhi. Hivyo kwa mtu anaetaka kuwa mkulima au mkulima ambae hana ardhi ya kutosha na anataka kuanza shughuli za kilimo Tanzania anatakiwa atambue kuna mashamba yanayokodishwa. Sehemu nyingi za kilimo gharama hizi ni ndogo ambapo unaeza kupata ekari moja kwa wastani wa shilingi elfu 50. Msaada mwingine ni kuunda vikundi vya pamoja kama VIKOBA, vikundi hivi huundwa na mtu yoyoye kwa kujikusanya kuanzia watu 2 nakuendelea. Katika urahisi vikundi vya VIKOBA (Village Community Bank) ni vikundi vinavyoanzishwa kwa kuchangishana. Vinakua na kima cha chini cha mchango kama hisa mara nyingi ni kiasi kidogo kinachoweza kutolewa na kila mwanachama.
Mwanachama yoyote anaruhusiwa kukopa na kurudisha kwa riba ndogo sana isiozidi asilimia 10 ukilinganisha na asilimia hadi 25% za benki zinazo ambatana na dhamana.. Vikundi vya vikoba vinaweza kupiga hatua na kuunda SACCOS kwa ajili ya kupata misaada ya serikali. Kama mkulima ukijiunga huku unaweza kujipatia kipato kisicho na masharti yoyote kama ya riba za malipo.

Simplicity of VIKOBA gatherings not requiring a formal office (photo by the citizen)
Changamoto zinatoka wapi?
Licha ya jitihada zote hizo ni wazi kuwa bado mkulima anapata changamoto nyingi baadhi zikiwa; masoko ya mazao yasiotabirika, elimu ya magonjwa, uandaji bora wa mashamba na mitaji mdogo isiotosheleza kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa. Jitihada ni nyingi lakini wahitaji ni wengi. Ndio maana tunaona jitihada hizi zinafikia wakulima kwa mfumo wa vikundi na sio mkulima mmoja mmoja. Katika taswira nyingine, Tanzania ikiwa mtekelezaji wa soko huria la biashara, inapambana na ushindani mkubwa kwenye masoko yake na kilimo ni mojawapo ya sekta zinazopokea ushindani huo. Kuna bidhaa za kilimo zinazotoka nchi za nje na kuuzipa ushindani bidhaa za ndani. Kama moja ya sababu, Tanzania haina viwanda vya kutosha kwa ajili ya usindikaji na uzalishaji wa bidhaa zitokanzo na kilimo. Bidhaa hizi zinanyima utumiaji wa bidhaa zote za wakulima wa ndani katika mnyororo wa kilimo
Hamasa kwa Mkulima
Wakulima sanasana vijana wamehimizwa kuijikita katika kilimo na muamko umezidi kuongezeka kwani ajira za maofisini haziwezi kutosheleza idadi ya nguvukazi iliopo kwenye nchi. Zamani kilimo kilikumbwa na changamoto ya mvua chache, tafiti zilikua zipo kwa kiasi kidogo na mbinu za kisasa zilikua hazijawa maarufu. Hivi sasa wakulima wanaowekeza kwenye kilimo cha kisasa wanapata matokea ya uakika ya mavuno. Hii ndio sababu inayopelekea wimbi kubwa la vijana kuanza kurudi kwenye sekta hii ambayo imeekewa mikakati kama sera ya uchumi wa viwanda ili kumkomboa mkulima. Changamoto zipo ila kwa umakini na nia madhubuti matokeo chanya yameendelea kupatikana kwa wakulima nchini Tanzania.

Unataka kuwa mchangiaji? Tuulize swali tupe maoni au pendekezo juu ya mada hii au mada ambayo ungependa kuiona kwenye makala ijayo.Tuandikie kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Pia usiache kutufuata kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii.

Umependa ulichokisoma? Usisahau kusifia chapisho hili!
Unaweza pia kutuambia stori yako ama kuwakilisha maoni yako kwenye upande wa maoni hapo chini
Umependa ulichokisoma?
Usisahau kusifia chapisho hili!

Unaweza pia kutuambia stori yako ama kuwakilisha maoni yako kwenye upande wa maoni hapo chini
Je! Unapenda Humaniq Farm?
Jiunge na uwe wa kwanza kujua kuhusu machapisho mapya
Made on
Tilda