Write Close
Close
Contact us!
Njia 5 za kutengeneza kipato kupitia kilimo
Hatua ya kuanzia au nafasi ya kupanua

English | Swahili
Kilimo ni mfumo wa uzalishaji wa mazao kwenye mashamba, uzalishaji ambao hujumuisha mimea, wanyama na ufugaji wa samaki. Kilimo ni mfumo ambao hujumuisha shughuli tata ambazo ni kulima, kukuza, kuvuna na kuuza. Tanzania na East Afrika kwa ujumla inajihusisha na uzalishaji wa mazao ya aina nyingi kama vile nafaka, mikunde, mizizi, mazao ya mafuta, mazao ya asili, matunda, mbogamboga, maua na viungo.

Yafuatayo ni 5 mawazo yanayoweza tumika na anayetaka kuingia katika kilimo au anayetaka kupanua kilimo chake.
Uzalishaji Wa Vitunguu Maji Na Kuuza Katika Soko La Ndani Na Nje
Vitunguu maji ni zao ambalo lina matumizi makubwa sana katika maisha ya watanzania, ambapo hutumika karibia kila siku katika mapishi na kama tiba. Vitunguu maji hutumika katika kutungenezea supu, kachumbari, kiungo cha mboga, samaki na nyama. Vitunguu maji Tanzania hulimwa Tanga, Morogoro, Arusha na Singida.

Changamoto zilizopo katika zao hili ni pamoja na gharama kubwa za uzalishaji, uhaba wa maeneo ya kuzalishia, ushambuliwaji mkubwa wa magonjwa na uhaba wa elimu juu ya uzalishaji wa zao hili kwa watanzania wengi. Ni zao ambalo wakulima inabidi wazalishe kwasababu ni rahisi kupanda, kuvuna, kusafirisha na kuuza kwasababu ni moja kati ya mazao ambayo huhitajika kwa sana.

Anayeanza kuzalisha vitunguu au anayetaka kupanua biashara yake ya uzalishaji wa vitunguu anatakiwa afanye mambo yafuatayo tafuta mbegu bora za vitunguu ambazo zina soko kubwa sehemu mbalimbali kwamfano vitumngu vyekundu, zalisha vitunguu eneo ambalo ni rahisi kufikika kwa usafiri, jaribu kupunguza gharama za uzalishaji kadri uwezavyo haswa kwa kulima hekari nyingi na vile vile tafuta masoko mbalimbali ili kuweza kupata soko lenye bei nzuri ya kuuzia.
Uzalishaji Wa Mihogo Kwa Soko La Ndani Na Soko La Nje

Mihogo ni zao ambalo hutemewa na wakulima wengi katika sehemu kubwa ya nchi. Tanzania hutumika kwa kiasi kidogo na sehemu ya kuliwa haswa ni viazi vyake vilivyo na wanga kubwa sana halafu ni majani yake yenye protini na vitamini.

Mihogo Tanzania hulimwa zaidi katika kanda za kusini na maeneo yaliyopo kwenye mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari na ndio chakula ambach huliwa kwa wingi kuliko vyakula vingine. Uzalishaji wa mihogo unafaida kubwa sana kwa sababu ni zao ambalo hustahili ukame na linahitaji gharama ndogo tu kwahiyo ni fursa ya kipekee kwa wanatafuta mawazo ya kuanzisha biashara kuanza uzalishaji wake.
Vile vile uzalishaji wa mihogo hukabiriwa na changamoto kubwa sana ya kushambuliwa na magonjwa na wakulima wamekuwa wakikwepa kutumia mbegu za kisasa za mihogo na kuendelea kutumia za zamani. Zao la mihogo limepata soko kubwa sana nchini China kutokana na mkataba uliosainiwa kati ya china na Tanzania la kufungua soko la China la mihogo, hivyo basi ni fursa ya kipekee ya watanzania kuweza kujipatia kipato.

Kwa watu wanaotaka kujiingiza na uzalishaji wa zao hili au ambao wanataka kupanua zaidi faida wanaweza kutafuta mbegu bora za mihogo kwa kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa kilimo wa eneo husika, kusindika mihogo kwa kuibadilisha fomu kama vile kutengeneza chips za mihogo na vitu mbalimbali na pia kuboresha uhifadhi ili kuweza kuuza kipindi ambacho mihogo huadimika au kusafirisha katika maeneo ambayo hawajihusishi na uzalishaji wa mihogo.
Uzalishaji Wa Mboga Za Majani Kwa Uuzaji wa Soko La Ndani
Mboga za majani ni sehemu za mimea ambazo hupikwa kama chakula na kuliwa na binadamu. Mboga za majani ambazo hulimwa Tanzania ni kama vile spinachi, kabeji, mchicha na sukumawiki. Mboga za majani hulimwa karibia kila sehemu nchini Tanzania. Kutokana na ongezeko la uelewaji wa umuhimu wa kutunza na kulinda afya. Watanzania wengi wamehamasika kuhusu utumiaji wa mboga za majani hivyo imeweza kuongeza soko la mboga za majani zinazolimwa nchini.

Mboga za majani huzalishwa ndani ya siku chache kabla ya kupelekwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa hivyo kutokana na tabia za watanzania ni zao ambalo linaweza kufanywa na watu wa aina zote wakiwemo wenye ratiba zinazobana sana.

Changamoto kubwa inayoikabili ni uwepo wa magonjwa mbalimbali ambayo huweza kutibika. Mboga za majani zina soko kubwa sana ndani ya nchi kwasababu huweza kuuzwa kiurahisi katika sehemu mbalimbali ambazo zinauhitaji mkubwa sana kama vile kwa matumizi ya nyumbani, katika supermarket, katika hoteli kubwa za kulala wageni pamoja na hoteli za kitalii. Hivyo basi ni fursa muhimu sana ambayo huweza kuongeza vipato vya vijana kama wakijihusisha na uzalishaji wake.

Kwa mtu ambaye antaka kujiingiza katika uzalishaji wa mboga za majani anatakiwa aweze kuonana na watu ambao wanafanya huu uzalishaji ili aweze kujipatia weledi wa kutosha jinsi ya kuanza uzalishaji wake lakini akumbuke kutafuta sehemu ambazo anaweza kuuzia bidhaa zake pindi atakapo kua amezizalisha. Lakini kwa mtu ambaye anataka kupanua biashara yake anatakiwa asindike bidhaa zake, aziweke kwenye vifugashio vyake na aweze kuboresha eneo la kuhifadhia mazao yake
Uzalishaji Wa Mbao Na Kuuza Katika Maeneo Mbalimbali Ya Nchi
Mbao ni bidhaa ambayo imekua na uhitaji mkubwa sana katika karne hii ya ishirini na moja, kwa sababu ya kua na matumizi mengi muhimu kama vile kutengenezea thamani pamoja na kujengea nyumba kama kuelezekea nyumba. Kilimo cha miti Tanzania hufanyika mikoa ya Tanga, Iringa na Mororgoro.

Uwekezaji wa miti huchukua muda mrefu sana kabla ya kuanza kuvuna nah ii ndio changamoto kubwa sana ambayo watu wengi huikwepa, kwa mfano miaka minne kwa mikaratusi na Milingoti na miaka kumi kwa mipaina. Faida kubwa ya kilimo cha miti ni kwamba mbao hua na bei nzuri san katika uuzaji hali inayopelekea wanaojihusisha na kilimo hiki kua na kipato kikubwa sana.

Ili wakulima wanaotaka kujihusisha au wanaojihusisha na uzalishaji wa mbao wapate faida kubwa inabidi waboreshe maeneo ya uhifadhi yaani yawe ni rafiki kwa kuhifadhia mbao na yawe makubwa ili kuweza kuhifadhi mbao za kutosha, kuyatengeneza katika maumbo ambayo ni rahisi kuyasifirisha ili kupunguza gharama za usafirishaji, kutafuta soko katika maeneo ambayo huuzwa kwa bei nzuri na kuyasafirisha adi eneo ambalo unataka kuuzia. Kwasababu mbao ni rahisi kuuzika katika maeneo mengi sana kutokana na umuhimu wake katika shughuli za ujenzi.

Uzalishaji Wa Mpunga Na Kuuza Katika Soko La Ndani
Mpunga ni zao ambalo hukobolea na kutengenezamchele. Mchele ni punje za mpunga zinazokobolewa na mashine baada ya kuvunwa kabla ya kupikwa. Mchele ni miongoni mwa vyakula ambavyo hupendelewa zaidi kuliwa na watanzania wengi. Mikoa ambayo hulima zaidi mchele Tanzania ni Morogoro, sumbawanga, Mbeya, Iringa, Pwani na Tabora.

Changamoto kubwa ambayo wakulima wa mpunga hukutana nayo ni utegemezi wa mvua. Faida kubwa ya uzalishaji wake ni kwamba kuna soko kubwa la mpunga ndani na nje ya nchi. Hivyo ni fursa ambayo vijana wengi wanaweza kujiingiza ili waweze kujitengenezea kipato cha kutosha.

Vitu vya muhimu ambavyo mkulima wowote anajihisha au anayetaka kujihusisha na azalishaji wa mpunga inatakiwa atafute mbegu ambayo inahitajitaka kwa wingi na inabei kubwa ili aweze kupata faida kubwa atakapozalisha, aboreshe hifadhi yake ili aweze kuuza kipindi ambacho mpunga utakua na bei kubwa, afanye usindikaji yeye mwenyewe kwa kuukoboa na kuweka kwenye vifungashio na pia asafirishe adi maeneo ambayo mchele unauzwa kwa bei kubwa ya kuridhisha

Kama ujumbe huu umekua na manufaa yeyote kwako usisahau kubonyeza "like" na kama unamapendekezo yoyote au ungependa tuongeze mawazo mengine usisahau kukoment hapo chini.

Ni mimi mwandishi wako
HAMISI SALUMU NAMPOTO

AGRICULTURAL ECONOMIST
Umependa ulichokisoma? Usisahau kusifia chapisho hili!
Unaweza pia kutuambia stori yako ama kuwakilisha maoni yako kwenye upande wa maoni hapo chini
Umependa ulichokisoma?
Usisahau kusifia chapisho hili!

Unaweza pia kutuambia stori yako ama kuwakilisha maoni yako kwenye upande wa maoni hapo chini
Je! Unapenda Humaniq Farm?
Jiunge na uwe wa kwanza kujua kuhusu machapisho mapya
Made on
Tilda